SURA YA 05 / 08 · PRESENTATIONS & BODI
Kuandaa Mpangilio wa Slides za PowerPoint, Bodi, na Pitch Decks
Jinsi ya kutumia AI kupanga mtiririko wa slides 8–10 zenye mvuto na kujiandaa kuwasilisha mbele ya uongozi au wateja.
JIBU LA HARAKA · MUHTASARI WA SURA
Msingi wa sura hii kwa sekunde 30.
Wasilisho bora la PowerPoint (Presentation) halipaswi kujazwa aya ndefu za maandishi kwenye slide moja. Tumia kanuni ya 'Wazo Moja Kuu kwa Kila Slide' (1 Idea per Slide, si zaidi ya vipengele 4 kwa slide), na utumie AI kukuandalia muundo wa slide kwa slide: Kichwa cha Slide kinachobeba ujumbe mkuu (Action Title), Bullet Points 3 fupi za kuonekana kwenye skrini, na Maelezo ya Mzungumzaji (Speaker Notes) utakayoyasema kwa mdomo.
Wafanyakazi wengi wanapoambiwa waandae PowerPoint Presentation kwa ajili ya kikao cha menejimenti au wateja, wanakili ukurasa mzima wa Word na kuubandika kwenye slide moja kwa herufi ndogo sana, kisha wanasimama mbele kusoma neno kwa neno. Hilo linawachosha wasikilizaji ndani ya dakika 2!
Mpangilio wa Slides 8 wa Wasilisho la Kitaalamu (Executive Slide Deck)
| Namba ya Slide | Jina la Slide | Kinachopaswa Kuonekana Kwenye Skrini |
|---|---|---|
| Slide 1 | Kichwa na Lengo Kuu | Jina la mada, mwasilishaji, na lengo la wasilisho kwa sentensi 1 |
| Slide 2 | Muhtasari wa Uamuzi (Executive Summary) | Jibu kuu au matokeo makuu 3 unayotaka wasikilizaji waondoke nayo |
| Slide 3 | Hali ya Sasa / Tatizo (Current State) | Takwimu 2–3 zinazoonyesha kwa nini jambo hili linahitaji umakini sasa |
| Slide 4 | Uchambuzi / Chaguzi (Insights & Options) | Jedwali fupi au mlinganisho wa njia za kutatua changamoto |
| Slide 5 | Suluhisho Linalopendekezwa (Proposed Plan) | Hatua 3–4 za mpango unaopendekeza |
| Slide 6 | Bajeti na Faida (Cost vs ROI) | Gharama inayohitajika dhidi ya faida au akiba itakayopatikana |
| Slide 7 | Ratiba ya Utekelezaji (Timeline & Owners) | Mstari wa muda (Wiki/Mwezi) na nani anasimamia nini |
| Slide 8 | Hitimisho & Maamuzi Yanayohitajika | Maswali na uamuzi mahsusi unaoomba uidhinishwe kwenye kikao hicho |
Kanuni ya "Action Titles" Kwenye Slides
Badala ya kuandika kichwa cha slide "Mauzo ya Robo Mwaka", andika kichwa kinachotoa ujumbe: "Mauzo ya Robo ya Tatu Yamekua kwa 18% Kutokana na Masoko ya Kidijitali."
HATUA KWA HATUA OFISINI KWAKO
Hatua 4 za kuandaa PowerPoint Presentation kwa dakika 15
- Mweleze AI lengo la wasilisho lako, nani atakuwa msikilizaji (Mkurugenzi, Bodi, Wateja), na muda ulionao
- Mtume AI akutengenezee mpangilio wa Slides 8–10 ukiwa na Action Title na Bullet Points 3 fupi kwa kila slide
- Omba Speaker Notes (maelezo ya kuongea kwa mdomo) kwa kila slide ili usilazimike kujaza maandishi mengi kwenye skrini
- Weka vipengele hivyo kwenye PowerPoint, Canva, au Google Slides na uongeze chati au jedwali safi
ONA TOFAUTI KWENYE KAZI ZA OFISI
Mfano halisi: Mbinu ya zamani vs Mbinu ya kitaalamu kwa msaada wa AI.
Slide 3: Ripoti ya Idara ya IT Idara ya IT imefanya matengenezo ya kompyuta 45 mwezi huu na pia tumeona kuwa mfumo wa zamani wa mtandao unakata mara kwa mara hasa mvua ikinyesha na kusababisha wafanyakazi kushindwa kutuma ripoti kwa wakati hivyo tunahitaji kununua vifaa vipya vya mtandao...
SLIDE 3 TITLE: Maboresho ya Mtandao Yatapunguza Muda wa Kukwama kwa Kazi kwa 80% KWENYE SLIDE (Bullets 3): • Kompyuta 45 zimefanyiwa matengenezo (100% ya lengo la mwezi) • Changamoto kuu: Kukatikakatika kwa mtandao kunapoteza saa 6 za kazi kila wiki • Suluhisho: Kuweka Backup Router (Gharama: TZS 450,000) SPEAKER NOTES (Cha kuongea): Kama mnavyoona kwenye slide hii, timekamilisha matengenezo ya kompyuta zote, na sasa hatua moja itakayookoa saa 6 kila wiki ni...
Slide ya pili ni safi machoni, inasomeka kwa sekunde 5, na inampa mwasilishaji maelezo ya kuongea (Speaker Notes) yanayoonyesha umahiri mkubwa.
PROMPTS 3 ZA KAZI ZA OFISINI SASA HIVI
Badilisha, nakili na utumie kwenye ChatGPT, Gemini au Claude.
Chagua mojawapo ya prompts hapa chini, weka maelezo ya idara yako, safu za Excel, au mada ya kikao kwenye mabano [...], kisha bonyeza Nakili Prompt.
Kazi (Task): Niandalie mpangilio kamili wa wasilisho (Presentation) lenye slides 8 kwa ajili ya [TAJA KIKAO AU MADA YA WASILISHO]. Muktadha (Context): Walengwa wanaonisikiliza ni [WAKURUGENZI / BODI / WATEJA / WAFANYAKAZI]. Ujumbe mkuu na takwimu ninazotaka kuwasilisha ni: [TAJA HOJA ZAKO KUU]. Muundo wa Jibu (Output Format): Kwa kila slide nipe: (1) Action Title, (2) Bullet points 3 fupi zisizozidi maneno 10 kila moja kwa ajili ya kuweka kwenye slide, (3) Pendekezo la mchoro/jedwali, na (4) Speaker Notes za kusema kwa mdomo. Lugha (Language): Kiswahili cha Tanzania. Kanuni ya Ukweli: Tumia taarifa nilizotoa pekee. Kama kuna bei, tarehe, au sharti muhimu linalokosekana, weka alama ya kuuliza badala ya kubuni.
Badilisha maneno yenye mabano [...] kulingana na mteja wako kisha nakili.
ZOEZI LA OFISINI & KUJIPIMA
Kamilisha mpango wako wa kazi za ofisini kwenye sura hii.
Andika angalau sentensi moja fupi kuhusu jinsi utakavyotumia mbinu hii.
Kamilisha hatua hii
Andika zoezi lako na ujibu swali kwa usahihi ili kukamilisha sura hii.